Header Ads

Header ADS

Wananchi wajitolea kuweka alama za barabarani

Wananchi  wa Kata ya  Lemara eneo la Nanenane  jijini Arusha wameamua kujitolea kwa  hali na mali kuweka  alama za  vivuko viwili vya waenda kwa miguu katika barabara inayoingia katikati ya jiji kwenye eneo linalodaiwa kutokea  ajali za mara kwa mara  na   kusababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha .

Tukio Hilo limetokea eneo la nanenane na kushuhudia  wakazi wa eneo hilo wakichangishana fedha kwa ajili na kuweka alama hizo huku mafundi wakiendelea  na kazi ya kuweka alama hizo ambazo zinatajwa kua ni suluhisho la kuzuia  ajali kutokea katika  eneo hilo.

Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia hatua waliochukua ya kujitolea kwa michango yao wakishirikiana na diwani wao nibaada ya eneo hilo kukidhiri ajali za mara kwa mara ambazo wakati mwingine zinaepukika.

Alfredy Maulid na Pascal Silvery ni  wakazi wa kata ya lemara walisema upatikanaji wa kivuko hicho  ni mkombozi mkubwa  hasa watoto wa shule kuvuka kwa amani kwakua kipindi cha nyuma hali ilikua mbaya ya watu kupoteza maisha kwa kugongwa na magari.

Pascal alisema kuwa wanaamini kuwepo kwa alama hizo kutasaidia wanaovuka waweze kuvuka salama hususan wanafunzi ambao hupata adha kubwa wanapotaka kuvuka barabara.

Diwani wa Kata ya Lemara, Profesa  Raymond Mosha  alisema kuwa    ameungana na  wananchi  kutokana na  umuhimu wa eneo hilo  hawezi kuvumilia kuona watu wakiumia wakati wananchi wanaweza kujitoa na kufanikisha  jambo hilo .

“Ushirikiano kati ya Wananchi na Viongozi wao umeweza kufanikisha jambo hili muhimu ,tayari  tulishatoa taarifa uongozi wa Jiji umetoa ridhaa kwa wananchi kufanya jambo hili hivyo lina Baraka zote za jiji” Alisema Profesa Mosha

Dereva wa magari Johnson Mlay    alisema  hatua  iliyofanywa na wananchi  itawasaidia   kufuata sheria  ili kuepusha ajali zisizo za lazima.



No comments

Powered by Blogger.