Header Ads

Header ADS

Facebook, WhatsApp na Instagram Zapata Tatizo la Kimtandao

Facebook, WhatsApp na Instagram Zapata Tatizo la Kimtandao
Mtandao wa kijamii wa Facebook kwa sasa inakumbwa na hali mbaya zaidi ya mawasiliano kuwahi kutokea katika historia yake kwani huduma nyingi hazipatikani kote ulimwenguni.

"Tunafahamu kuwa baadhi ya watu hawana hawawezi kufikia app zinazohusiana na Facebook ," ilisema taarifa iliyotolewa na Facebook.

Haijabainika wazi ni nini kinachosababisha shida hiyo.

"Tunafanya kila juhudi kushughulikia tatizo lililopo haraka iwezekanavyo."

Kando na Facebook yenyewe, huduma za Messenger na Instagram zimetatizwa.

Mara ya mwisho Facebook ilijipata katika hali hiyo ilikuwa mwaka 2008 wakati mtandao huo ulikuwa na watumiaji milioni 150 -ikilinganishwa na sasa ambapo watumiaji karibu wanakadiriwa kuwa karibu bilioni 2.3 kwa mwezi.

Kampuni ya Facebook imejibu uvumi unaoendelea mitandaoni kuwa huenda mtandao huo maarufu duniani umedukuliwa.

Inasema hali hiyo haijatokana na shambulio lolote la kimtandao


Inakadiriwa kuwa tatizo hilo lilianza kukumba mtandao huo siku ya Jumatano.

Japo huduma ya Facebook ilionekana kuwa sawa watumiaji wake waliripoti kuwa na hawawezi kutuma ujumbe.

Watumiaji wa Instagram hawawezi kufikia ujumbe mpya huku wale wanaotumia huduma ya Facebook Messenger kupitia kompyuta pia wakikabiliwa na changamoto sawia na hiyo

No comments

Powered by Blogger.